#HABARI: Madiwani 27 wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wamemchagua tena Ndugu Twalib Lubandamo ‘Takus’ kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, baada ya kupata kura zote 27, sawa na asilimia 100, ambapo baada ya kutangazwa mshindi, Takus amewataka Madiwani wapya walioapishwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kiapo chao, huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha umoja na ustawi wa Halmashauri.
Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbarali, Frank Sichalwe, aliyebainisha kuwa Takus—Diwani wa Kata ya Itamboleo, amepata ridhaa ya Madiwani wote kwa mara ya pili mfululizo.
Katika uchaguzi huo, Madiwani wamemchagua pia Chuki Jeremiah kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri kwa asilimia 100 ya kura zote.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.