Mawakala watano wa mabasi ya mikoani wanaohudumia katika kituo cha mabasi ya mikoani na nje ya nchi cha Magufuli kilichopo Mbezi, Dar es Salaam wamekamatwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa tuhuma za kufanya ulanguzi wa bei za tiketi wakati huu ambapo uhitaji wa kusafiri umeongezeka maradufu.
Esterbella Malisa ameshuhudia ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo kituoni hapo.
Mhariri @moseskwindi