😱🚗| MBAPPE HAWEZI KUENDESHA GARI !?
Mwanzoni mwa msimu, Kylian Mbappé alipokea BMW yake ya kifahari iliyotengenezwa maalum kupitia ushirikiano wa Real Madrid na kampuni hiyo — lakini bado HAIWEZI KUENDESHA! 🚙🥲
Akiwa na umri wa miaka 26, Mbappé bado hajafaulu mtihani wa udereva na kisheria hawezi kukaa siti ya dereva aendeshe gari😳📚.
Ameshawahi kueleza kuwa leseni haikuwa kipaumbele kwa sababu taaluma yake ya soka ilianza mapema sana. Kwa sasa, anategemea wazazi wake au dereva binafsi kumpeleka mazoezini na kwenye matukio maalumu. 🐢