Ripoti iliyotolewa na The Global Economic Inequality (GEI) kuhusu ukosefu wa usawa wa kiuchumi duniani imeonya pengo linaloongezeka kati ya matajiri na maskini na haja ya dharura la kushughulikia mgogoro huu, ikisema: asilimia 10 ya idadi ya watu duniani wanamiliki asilimia 75 ya utajiri wote wa dunia.

Gazeti la The Guardian la Uingereza limeandika kuwa kwa mujibu wa ripoti ya The Global Economic Inequality (GEI), ukosefu wa usawa katika uchumi wa dunia umefikia kiwango kinachowajibisha kuchukuliwa hatua za haraka. Ripoti hiyo inasema, chini ya watu 60,000, ambao ni sehemu moja ya elfu ya asilimia moja ya idadi ya watu duniani, wanamiliki mara tatu ya utajiri wote wa nusu ya watu maskini zaidi ya idadi ya watu duniani.

Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya kimataifa ya The Global Economic Inequality, inayochapishwa kila baada ya miaka minne kwa ushirikiano na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, data iliyokusanywa na watafiti 200 inaonyesha kwamba asilimia 10 watu matajiri zaidi duniani hupata kipato cha zaidi ya asilimia 90 nyingine, huku nusu ya idadi ya watu duniani ikipata chini ya asilimia 10 ya mapato yote ya dunia.

Matokeo mengine ya ripoti hiyo ni kwamba 10% ya watu matajiri zaidi duniani wanamiliki 75% ya utajiri wa dunia, huku nusu maskini zaidi ya watu wakimiliki 2% tu ya utajiri wote wa dunia. Kwa hivyo, katika maeneo yote ya dunia, asilimia moja ya juu ya jamii ina utajiri zaidi kuliko asilimia 90 nyingine ya watu, na ukosefu huu wa usawa unaongezeka kwa kasi.

Thomas Piketty, mchumi mashuhuri wa Ufaransa na mwandishi mwenza wa ripoti hiyo, amesema kuwa ingawa ukosefu wa usawa umekuwa sifa kuu ya uchumi wa dunia kwa muda mrefu, lakini kuanzia mwaka huu wa  2025 hali hiyo imefikia hatua ambayo inahitaji mazingatio ya haraka.

Amesisitiza kuwa: “Kutokuwepo usawa si tu kwamba ni ukosefu wa haki, lakini pia kunaathiri uthabiti wa demokrasia na kuifanya sayari yetu isiwe mahali pa kuishi.”

Ripoti hiyo pia imetilia mkazo mchango muhimu wa matajiri katika mabadiliko ya tabianchi, ikisema: “Watu matajiri pia wanachochea mgogoro wa tabianchi kupitia uwekezaji wao.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *