#HABARI: Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuongeza kasi, uwajibikaji na ubunifu katika utekelezaji wa miradi yake ya kimkakati, ikiwemo ujenzi wa Mtanda Commercial Complex unaotekelezwa mkoani Lindi kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.26.
Akizungumza mkoani humo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, Mhe. Mmuya amesema Shirika hilo limepewa dhamana kubwa ya kuchochea maendeleo ya taifa, hivyo linapaswa kufanya kazi kwa ufanisi, weledi na kasi inayolingana na matarajio ya Serikali.
Amewasisitiza viongozi wa Shirika hilo kutumia vyema mitandao ya kijamii kutangaza miradi na fursa zake ili kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara, hatua itakayoongeza mapato ya Shirika na kuliongezea ushindani katika soko la majengo.
Kadhalika Naibu Waziri huyo ameelekeza Shirika hilo kuhakikisha linafunga kamera za usalama (CCTV) katika jengo hilo kabla ya kuanza kutumika kwa shughuli za kibiashara, ili kulinda mali na watumiaji wa majengo hayo.
Kwa upande wake, Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi, Bw. Omary Makalamangi, amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika ifikapo Januari 1, 2026.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania