#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuteketeza shamba la bangi lenye ukubwa wa hekta 2.5 katika eneo la Mnyika, Kijiji cha Chonwe, Wilaya ya Kipolisi ya Ruhembe, Kilosa. Operesheni hiyo ni sehemu ya mikakati endelevu ya jeshi hilo katika kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya mkoani humo, ikilenga kuzuia uzalishaji na usambazaji wa bidhaa hizo haramu zinazoharibu nguvu kazi ya taifa.

Katika msako huo, Polisi wamemkamata mtuhumiwa mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Festo Stephen katika eneno linalohusishwa na shamba hilo. Wakati mtuhumiwa huyo akiendelea kuhojiwa, jeshi hilo limebainisha kuwa uchunguzi mkali na msako dhidi ya mmiliki mkuu wa shamba hilo bado unaendelea ili kuhakikisha wote waliohusika wanachukuliwa hatua kali za kisheria.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *