Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Makame, ametoa siku 14 kwa uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha jengo la mama na mtoto linaanza kutumika mara moja.
Jengo hilo ni miongoni mwa majengo yanayokarabatiwa kwa fedha za ruzuku ya Serikali zaidi ya shilingi milioni 900. Awali, ukarabati wa jengo hilo ulipangwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu, hata hivyo hadi sasa kazi zimekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
Makame ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea hospitali hiyo na kukagua maendeleo ya ukarabati unaoendelea, akisisitiza kuwa ucheleweshaji wa kuanza matumizi ya jengo hilo unaathiri upatikanaji wa huduma bora za afya kwa mama na mtoto.
✍Joyce Lyanda
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates