#HABARI: Mamia ya wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini wamefururika katika eneo la Soko la Uhindi kwa lengo la kuuaga mwaka 2025 na kuupokea mwaka mpya wa 2026. Mkusanyiko huo uliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuimarisha mshikamano, upendo na umoja miongoni mwa wakazi wa jiji hilo wanapovuka kuelekea msimu mpya.

Katika kuelekea kilele cha mapokezi hayo, wananchi waliendelea kupata burudani mbalimbali huku wakijumuika na viongozi wao, akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo, Mheshimiwa Patrick Mwalunenge. Huku mazingira ya soko hilo yamejaa bashasha na shamrashamra, kila mmoja akisubiri kwa hamu dakika za kuingia mwaka mpya akiwa na matumaini makubwa.

Akizungumza na hadhara hiyo, Mkuu wa Wilaya, Solomon Itunda, amewasihi wananchi kusherehekea kwa kiasi na kuepuka matumizi ya vilevi kupita kiasi. Amesema kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kuepuka matendo yasiyofaa na kuhakikisha wanauvuka mwaka salama bila kuingia kwenye matatizo au uvunjifu wa sheria.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *