MTWARA: MADIWANI wa Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara wametakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro itakayopelekea taharuki katika maeneo yao na badala yake waibue shughuli za kimaendeleo.

Rai hiyo imetolewa wakati wa kuhitimishwa mafunzo elekezi ya siku mbili kwa madiwani hao yaliyofanyikwa katika manispaa hiyo yaliyotolewa na TAMISEMI lengo ni kuwajengea uwelewa ili waweze kutekeleza vema majukumu hayo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Katibu Tawala Wilaya ya Mtwara Richard Mwalingo amesema madiwani hao wakayafanyie kazi yote waliyofundishwa na kujizuia kuwa sehemu ya kuibua migogoro isiyo kuwa na tija.

‘’Tusiende kutoa kauli ambazo zitaleta taaruki kwenye maeneo yetu sisi tumekuwa sehemu ya serikali na ukienda kusema lolote linalozua taaruki maana yake itakuwa unajikosoa wewe mwenyewe, sasa tusiwe viongozi wa kwenda kuzua migogoro na kusababisha taaruki na kuleta shida kwenye maeneo yetu,”amesema Mwalingo.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Mwalimu Hassan Nyange amewasisitiza madiwani hao kuwa katika majukumu hayo wazingatie suala la mahusiano mazuri kwa watalaamu na wananchi kwenye kata zao ili waweze kutekeleza kikamilifu majukumu yao ili watapoondoka waache alama ya jitihada na matunda ya uongozi huo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo diwani wa kata ya chuno Mariamu Chimbwahi ‘’Kupitia mafunzo haya nimejifunza mambo mengi mfano suala la mahusiano mazuri na wananchi na kushirikisha mambo mbalimbali hasa pale inapotekea miradi ya maendeleo ya kata”.

Aidha, miongoni mwa mada zilizotolewa kwa madiwani katika mafunzo hayo ikiwemo suala la mahusiano mazuri kwa   wataalamu na wananchi, wawe na uwezo mkubwa wa kujenga hoja katika vikao mbalimbali vya maendeleo ya kata (WDC), maamuzi yenye maslahi na wananchi na mengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *