Rais wa Marekani Donald Trump amesema Marekani “itaiongoza” Venezuela hadi “mabadiliko salama, sahihi na ya busara” ya kisiasa yatakapohakikishwa, baada ya mashambulizi ya Marekani kusababisha kukamatwa kwa Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro.
Makampuni ya mafuta ya Marekani pia yatarekebisha “miundombinu iliyoharibika” ya mafuta Venezuela na “kuanza kupata pesa kwa ajili ya nchi,” Trump alisema.
Marekani ilianzisha mashambulizi dhidi ya Venezuela siku ya Jumamosi ambapo Maduro na mkewe, Mke wa Rais Cilia Flores, walikamatwa na vikosi vya Marekani na kuondolewa nchini humo.
Venezuela ilitangaza hali ya hatari ya kitaifa na kulaani “uchokozi wa kijeshi” wa Marekani, huku makamu wa rais wa nchi hiyo akisema Maduro ndiye kiongozi wake pekee.
Maduro na Flores walisafirishwa kutoka mji mkuu wa Caracas kwa helikopta ya Marekani mapema asubuhi ya Jumamosi na kutangazwa baadaye kuwa wamefikishwa New York.
Baadaye walisafirishwa hadi Kituo cha Jeshi la Wanamaji cha Marekani cha Guantanamo Bay huko Cuba kabla ya kuhamishiwa kwenye ndege nyingine kuelekea Jimbo la New York, na kisha kupelekwa kwa helikopta hadi Kituo cha Magereza cha Jiji la New York huko Brooklyn.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani Pam Bondi alisema Maduro na Flores wameshtakiwa katika Wilaya ya Kusini mwa New York.
Rais Maduro na mke wake wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kufanya ugaidi wa dawa za kulevya na kuingiza nchini humo kokeni, kumiliki bunduki za rashasha na vifaa vya uharibifu dhidi ya Marekani.
“Hivi karibuni watakabiliwa na mkono wa sheria katika mahakama za Marekani,” Bondi aliandika kwenye X.
Hapo awali, Maduro alikanusha vikali kuwa kiongozi wa kundi la wahalifu na ameishutumu Marekani kwa kutumia “vita vyake dhidi ya dawa za kulevya” kama kisingizio cha kujaribu kumng’oa madarakani na kutwaa akiba kubwa ya mafuta ya Venezuela.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kuwasili kwa Maduro jijini New York, Trump alisema: “Biashara ya mafuta nchini Venezuela imekuwa ik