Klabu ya Manchester United ya England imemfuta kazi kocha mkuu wa Ruben Amorim, ambaye amekuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha takribani miezi 14 akiwa Old Trafford.
Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na matokeo yasiyoridhisha kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo na changamoto za ndani ya klabu licha ya kufika fainali ya Ligi ya Europa msimu uliopita.
Aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo ambaye pia alikuwa kocha wa timu ya vijana, Darren Fletcher, ametangazwa kukaimu nafasi hiyo.
Fletcher ataiongoza timu kuanzia mechi ijayo wakati klabu ikiendelea kutafuta kocha wa kudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *