
Dakar – Mkutano wa usalama wa chakula umemalizika hivi karibuni nchini Senegal, Mkurugenzi Mkuu wa Africa Food Systems Forum (AFSF), Amath Pathe Sene, akitumia mkutano huo kuweka mikakati thabiti ya kubadilisha sekta ya kilimo na chakula barani kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao, shabaha ya Pathe ikilenga kulisha Afrika, kuunda nafasi za ajira na kuwawezesha wanawake na vijana.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Sene anakiri kuwa bara bado linakabiliwa na changamoto ya kujilisha, huku likitegemea uagizaji mkubwa wa chakula, wakati mamilioni ya vijana wa Afrika wakibaki bila ajira.
Kulisha Afrika, kuunda ajira kwa vijana na wanawake — huo ndiyo mpango. Unaweza kuonekana rahisi kwa maneno, lakini changamoto kubwa ni utekelezaji wake,
Vijana na mageuzi ya sekta ya kilimo
Kwa mujibu wa Sene, vijana wa Afrika hawapaswi kuonekana tu kama wanufaika, bali kama wabunifu na wenye kuleta suluhu. Akimnukuu Rais wa Rwanda, Paul Kagame, aliyesema: N
i rahisi zaidi kumuunga mkono mtu anayesuluhisha matatizo kuliko yule anayesubiri wengine wamsaidie.
Aliwahimiza vijana kuchukua nafasi za uongozi, kukumbatia ubunifu na kuangalia kilimo si tu kama fursa ya biashara bali pia kama njia ya kujenga utajiri.
Sera na Ufadhili
Sene aliwasifu viongozi wa Afrika kwa kuonyesha nia ya kisiasa, akitaja mawaziri na wakuu wa nchi wanaoshiriki kikamilifu katika kuunda ajenda ya usalama wa chakula. Hata hivyo, alionya kuwa “sasa tunapaswa kusonga mbele zaidi ya maneno na kuzingatia utekelezaji.”
Kuhusu ufadhili, Sene anasisitiza kuwa changamoto halisi si ukosefu wa fedha bali ni upungufu wa miradi inayoweza kuwekeza kibiashara. “Kama una mawazo makubwa na unaweza kupunguza hatari zake, fedha zitakuja,” alifafanua, akiwahimiza vijana wajasiriamali kuunda programu endelevu zilizo tayari kwa uwekezaji.
Nafasi ya Teknolojia
Mkurugenzi huyo Mkuu wa Africa Food Systems Forum (AFSF), alitaja teknolojia kuwa kiungo muhimu cha mageuzi ya kilimo Afrika. Kuanzia akili mnamba hadi matumizi ya droni, alihimiza bara kukumbatia na kupanua ubunifu. “Tunapaswa kusonga mbele. Ikiwa zana zipo, kwa nini tusubiri?” aliuliza, akisisitiza kuwa suluhu za kidijitali zinaweza kuharakisha maendeleo ya Afrika na uundaji wa ajira.
Kuipa Afrika Nafasi Mpya
Kwa kuwa na asilimia 60 ya ardhi inayoweza kulimwa duniani, mwanga wa jua wa kutosha na rasilimali za maji, Sene alieleza kuwa Afrika ina kila kinachohitajika kuwa ghala kuu la chakula duniani.
“Kile kinachohitajika ni nia ya kutumia rasilimali hizi kupitia programu za kitaifa na uongozi wenye maono,
Hata hivyo, alionya dhidi ya kujitenga. “Sisi ni soko la dunia. Tunajifunza kutoka kwa wengine, nao pia wanaweza kujifunza kutoka kwetu. La muhimu ni kujenga ushirikiano wa manufaa ya pande zote, unaotawaliwa na heshima na faida za pamoja.”
Majadiliano katika AFSF yalionyesha imani yake kuwa, iwapo vijana, wanawake na teknolojia watawekwa katikati, Afrika si tu kwamba itajilisha yenyewe bali pia itachangia pakubwa katika usalama wa chakula duniani.