#HABARI: Mtoto mwenye umri wa miaka 10 mkazi wa Kata ya Nyansha wilayani Kasulu mkoani Kigoma anaomba msaada wa matibabu baada ya kupata changamoto ya afya kwa kupoteza fahamu kwa zaidi ya miezi 8, kutolewa figo moja iliyoharibika na kuugua uti wa mgongo hali ambayo imepelekea kushindwa kusimama na kupoteza fahamu hivyo kulishwa chakula kwa kutumia mpira.

Mama mzazi wa mtoto huyo Bi. Lovenes Abdul, mkazi wa Nyansha wilayani Kasulu amesema kuwa inahitajika shilingi milioni tano ili mtoto huyo aweze kupata matibabu nje ya nchi hivyo kwa yeyote atakayeguswa anaweza kutoa msaada kwa kumpigia moja kwa moja katika namba yake ambayo ni 0755291193.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *