Wakazi wa Mkoa wa Morogoro wameishukuru Serikali kuanzisha Huduma za msaada wa Kisheria bila malipo kwa kuwa inasaidia wenye kipato cha chini na kupunguza migogoro.

Wakizungumza kwenye Kliniki ya siku mbili ya utoaji wa huduma za msaada wa kisheria, zinazotolewa bure kupitia taasisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), wakazi hao wameona Mpango huo uwe endelevu.

“Tunaishukuru Serikali kwa utaratibu huu unaogusa maisha ya Watanzania wengi, hususan wenye kipato cha chini wanaohitaji msaada wa kisheria,” amesema Amina Shabani.

Amina ameongeza kuwa ni muhimu kampeni hiyo ikaendelea na kuwafikia wananchi wengi zaidi, wakiwamo wanaoishi vijijini na maeneo ya pembezoni.

Naye Kombo Muya mkazi wa Kichangani, amesema amevutiwa na zoezi la utoaji wa vyeti vya kuzaliwa linaloendeshwa na RITA, kwa kuwa limeondoa usumbufu wa kufuatilia vyeti hivyo hasa kwa wananchi wanaoishi mbali na ofisi za taasisi hiyo.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mkoa kutoka RITA, Salima Ruhaka, amesema kupitia kliniki hiiyo wananchi wamepata huduma za vyeti vya kuzaliwa na lengo ikiwa kila Mtanzania anakuwa nacho.
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *