Makubaliano tete ya kuwa na serikali ya pamoja kati ya rais Salva Kiir na mpinzani wake wa muda mrefu Riek Machar, yamekuwa yakiyumba kwa miezi kadhaa sasa.

Makubaliano hayo yalivunjika baada ya Machar, aliye katika kizuizi cha nyumbani tangu mwezi Machi, kushitakiwa kwa makosa ya uhaini, mauaji na uhalifu dhidi ya binaadamu katika shambulizi lililofanywa na wanamgambo katika kambi moja ya kijeshi mwezi huo.

Wanamgambo hao wanaotokea kabila moja na Machar la Nuer, waliishambulia kambi ya kijeshi katika kaunti ya Nasir katika jimbo la Upper Nile, Kaskazini Mashariki mwa Sudan Kusini na kusababisha mauaji ya zaidi ya wanajeshi 250.

Chama chake kinasema hakuna ushahidi wowote wa kuonyesha Machar alihusika na shambulizi hilo na hatua ya kuwekwa katika kifungo cha nyumbani ni kinyume cha sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *