Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba, amesema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania Bara kwa robo ya kwanza ya mwaka 2026 inakadiriwa kufikia asilimia 6, huku Zanzibar ikitarajiwa kufikia asilimia 7.2.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Tutuba amesema kiwango cha riba cha Benki Kuu kimeendelea kubaki asilimia 5.75, na kuongeza kuwa sekta za kilimo, utalii, ujenzi na viwanda ndizo zinazoongoza kuchochea ukuaji huo.
Aidha, ameeleza kuwa mfumuko wa bei utaendelea kuwa katika lengo la asilimia 3 hadi 5, huku akiba ya fedha za kigeni ikiimarika kutokana na ongezeko la thamani ya dhahabu duniani na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la kimataifa.
#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi