@hamadaitz_ ameweka wazi kuwa alipokea kwa msisimko mkubwa taarifa za kuteuliwa na uongozi wa Clouds Media Group kufanya Hour Top ya mwaka mzima. Akizungumza kwenye kipindi cha #TheSpark na mtangazaji #missloloh, amesema kuwa alikuwa na ndoto hiyo kwa muda mrefu, huku akijipa changamoto ya kuandaa kiti ambacho watu hawatakisahau.
Amekiri kuwa alikuwa akifuatilia Hour Top za wasanii wengine na kusema moyoni, “Siku Clouds wakijichanganya na kuniita, nitafanya kitu ambacho hawatokuja kusahau ” Na hatimaye ndoto ikatimia.
Cc @missloloh_ @djfantastic255
#TheSparkShow #clouds26nyoosha