Mkurugenzi wa wa Masoko METL ametoa wito kwa wadhamini na wadau wa soko nchini kuwekeza kwenye ligi ya wanawake ambayo inakua kwa kasi nchini kwani kufanya hivyo kuna faida kwa ligi na nchi kwa ujumla.
Akizungumza katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge Jijini Dar es salaam ambapo Club ya Simba Queen imeshinda bao 3 kwa sifuri dhidi ya Timu ya Tausi FC Fatema amesema ni wakati sasa Kuwekeza nguvu kwenye soka la wanawake ili kuongeza tija katika Mchezo huo.
