#HABARI: Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeanza rasmi mchakato wa kuwarejesha nchini wakimbizi zaidi ya 80,000 walioko katika Kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma, ambao walikimbilia Tanzania tangu mwaka 1996.
Hatua hiyo inalenga kuwawezesha wakimbizi walioko tayari kurejea kwa hiari yao kushiriki katika ujenzi wa taifa lao na kuchangia juhudi za maendeleo baada ya zaidi ya miongo mitatu wakiwa uhamishoni.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa DRC, Bi. Ève Bazaiba, amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kwanza katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, ambapo alieleza kuwa serikali yake imejipanga kuhakikisha zoezi la urejeaji linakuwa salama, lenye heshima na kufanyika kwa hiari ya wahusika.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya mpango mpana wa serikali wa kuhimiza umoja wa kitaifa na kuimarisha maendeleo endelevu nchini humo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
