#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, ametoa pongezi za kipekee kwa Kamati ya Ukaguzi na Mapokezi ya Vifaa katika Shule ya Msingi Mahuta iliyopo Wilayani Tandahimba kwa uzalendo wao wa kukataa kupokea madawati yaliyo chini ya kiwango. Hatua hiyo imekuja baada ya kamati hiyo kubaini kuwa mzabuni aliyeshinda tenda hiyo alileta vifaa ambavyo havina ubora uliokusudiwa, jambo ambalo lingesababisha upotevu wa fedha za umma na kuhatarisha usalama wa wanafunzi.
Akipokea taarifa hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya madarasa na ufuatiliaji wa kuripoti kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza, Kanali Sawala amesisitiza kuwa msimamo huo wa walimu wa Mahuta Mjini unapaswa kuwa mfano kwa shule zingine mkoani humo. Amesema kuwa Serikali haitavumilia mzabuni yeyote anayejaribu kuhujumu jitihada za kuboresha elimu kwa kutoa vifaa hafifu, huku akiahidi kuendelea kusimamia kwa karibu thamani ya fedha katika miradi yote ya maendeleo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
