#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika shule za…#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika shule za…

#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, ametembelea na kukagua ujenzi wa miundombinu ya madarasa katika shule za msingi na sekondari ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara. Miradi hiyo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni tatu imelenga kukabiliana na ongezeko la wanafunzi, ambapo Kanali Sawala ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika ili madarasa yaanze kutumika muhula huu wa masomo.

Katika ziara hiyo, mkuu huyo wa mkoa amekagua ukarabati na ujenzi wa madarasa mapya akisisitiza umuhimu wa kukamilika kwa wakati ili kutoa fursa kwa wanafunzi kuanza masomo bila vikwazo. Hatua hii ni sehemu ya juhudi za mkoa kuhakikisha mazingira ya kufundishia na kujifunzia yanaboreshwa ili kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na shule hizo kwa mwaka huu wa masomo.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *