#HABARI: Mfugaji mmoja aliyetambulika kwa jina la Robert Ng’washa, mkazi wa Kitongoji cha Mshwamba (A) katika Kijiji cha Lunguza, wilayani Lushoto, amepoteza maisha baada ya kushambuliwa na kundi la tembo. Tukio hilo lilitokea wakati mfugaji huyo akiwa kwenye harakati za kumtafuta mbuzi wake aliyekuwa amepotea, ambapo alijikuta amezingirwa na wanyama hao na kushambuliwa hadi mauti yalipomfika.
Akizungumzia tukio hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kiwanda, Kata ya Mnazi, Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Wilaya ya Lushoto, Zakayo Ngioko, ameelezea masikitiko yake juu ya kuongezeka kwa migogoro kati ya binadamu na wanyamapori. Ngioko ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa mamlaka husika kuimarisha ulinzi na udhibiti wa wanyama hao wakali ili kunusuru maisha ya wananchi na mifugo yao ambayo imekuwa ikivamiwa mara kwa mara.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
