#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata watu watano kwa tuhuma za kumuua kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamza Malingumu Hussein (20) katika eneo la Lukobe, Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema kijana huyo aliuawa baada ya kudhaniwa kimakosa kuwa ni mwizi.

Hata hivyo, familia ya marehemu imeeleza kuwa Hamza alikuwa mgonjwa wa akili na alikuwa mgeni katika eneo hilo, jambo ambalo pia limethibitishwa na Jeshi la Polisi.

Mjomba wa marehemu, Ngwenje Mohamed, amesema kuwa Hamza, mkazi wa Wilaya ya Kilosa, alitoka nyumbani kwa mjomba wake mwingine, Nassib Ngwenje, mkazi wa Lukobe, majira ya saa tatu usiku bila watu wa nyumbani kufahamu, kisha akaanza kuzurura mitaani.

“Baada ya kupata taarifa kuwa amepigwa na kupoteza fahamu akidhaniwa kuwa ni mwizi, tulijaribu kumkimbiza hospitali kwa kutumia bajaji, lakini alifariki dunia akiwa njiani,” amesema Ngwenje.

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea, na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote mara uchunguzi utakapokamilika.
.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *