Jeshi la polisi mkoani Tabora linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kijana Dereva Bodaboda Hamisi Nchambi (27) ambaye aliuawa na kisha mwili wake kutelekezwa juu ya kaburi ukiwa umefungwa Kamba za plastiki shingoni,mikononi,na miguuni kwenye makaburi ya miemba mkoani Humo.

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP Costantine Mbogambi kukamatwa kwa watuhumiwa hao sita ambao kwa sasa wote wapo mikononi mwa Jeshi la polisi inatokana na msakao mkali uliofanywa na Askari na Makachero wa Jeshi hilo ambapo walifanikiwa kuwatia nguvuni watu hao ambao inadaiwa walikula njama pamoja kutenda unyama huo, wakiwa na pikipiki pamoja na simu ya marehemu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *