
Wakati fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikichezwa leo Jumapili, Januari 18, rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (AFCON), Patrice Motsepe, ametangaza siku ya Jumamosi Januari 17 kutamatika kwa CHAN, Mashindano ya Mataifa ya Afrika.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“CHAN ni shimo jeusi la kifedha lisilotabirika…” rais wa Shirikisho la Soka la Afrika alisema Jumamosi katika mkutano na waandishi wa habari. Wakati michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika sasa itachezwa kila baada ya miaka minne badala ya miwili, hii inaonyesha mabadiliko mengine makubwa kwenye kalenda ya soka ya Afrika.
“Naweza kuwaambia sasa,” alisema Patrice Motsepe, “Ligi ya Mataifa itachukua nafasi ya… [Anasita, kisha anaendelea].” Michuano yetu itapitiwa upya, na sasa naweza kuwaambia kwamba hakutakuwa na CHAN tena. CHAN haitakuwa muhimu tena.
Kwa sababu tunahitaji ushindani wa kutosha, lakini sio sana… na huu utakuwa wa kiwango cha dunia.
CHAN ambayo iliundwa mwaka wa 2009, ilikuwa sawa na Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani. Wazo lilikuwa kuwaonyesha wachezaji wa soka kutoka ligi za Afrika. Hii iliwezesha wachezaji kadhaa kujitokeza, kama vile Lamine Camara wa Senegal hivi karibuni au Ayoub El Kaabi wa Morocco, ambaye sasa ni mchezaji wa bora wa Atlas Lions.
Je, Ligi ya Mataifa itawezesha kugundua matumaini mapya makubwa ya soka ya Afrika? Ndiyo? Kulingana na Patrice Motsepe, ambaye alitangaza kwamba toleo la kwanza litafanyika mwaka wa 2029.