Baraza hilo limesema makubaliano hayo yaliyofikiwa siku ya Jumanne mjini Cairo yameangaliwa upya na kukubalika.

Hata hivyo limerejelea msimamo wa serikali ya Iran kwamba itafutilia mbali makubaliano hayo iwapo hatua za kichokozi zitachukuliwa dhidi ya nchi hiyo au vinu vyake vya nyuklia.

Siku ya Jumanne wiki iliyopita Mkuu wa shirika hilo la IAEA  Rafael Grossi  na waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi walifikia makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Misri.

Shirika hilo limekuwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Iran kwa wiki kadhaa juu ya ufufuaji wa uchunguzi huo.

Wasiwasi ulijiri baada ya Grossi kudai Iran ina zaidi ya kilo 400 za urani ambazo zimerutubishwa karibu kufikia kiwango cha kutengeneza silaha za nyuklia na hadi sasa nchi hiyo haijafichua mahali zilikohifadhiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *