Mbunge mmoja wa Marekani ameutaja uvamizi wa nchi hiyo dhidi ya Greenland kuwa utakuwa “vita dhidi ya Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi, NATO.”

Seneta wa Baraza la Wawakilishi wa chama cha Republican, Michael McCaul ameonya kwamba uvamizi wa Marekani dhidi ya Greenland utakuwa sawa na “vita” na Shirika la Mkataba wa Atlantiki Kaskazini (NATO).

Akizungumza na ABC News, McCaul amesema kwamba “kama Rais Donald Trump ataanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Greenland, suala hilo litadilisha kabisa Kifungu cha 5 cha NATO, na kimsingi ni kuanzisha vita na NATO yenyewe. Hatua hii hatimaye itasababisha kuvunjwa kwa NATO kama tunavyoijua.”

Kifungu cha 5 cha NATO kinasema kwamba shambulio la kutumia silaha dhidi ya mwanachama mmoja wa NATO linatambuliwa kuwa shambulio dhidi ya wanachama wote, na kwa mujibu wa kifungu hicho, kila mwanachama analazimika kuisaidia nchi inayoshambuliwa.

Wakati huo huo, gazeti la Uingereza la The Economist limeripoti kwamba niia ya Marekani ya kuitwaa Greenland katika kipindi hiki cha urais wa Trump imeibua mojawapo ya migogoro mikubwa zaidi ya ndani katika historia ya NATO, na kuweka misingi ya kuaminiana, ulinzi wa pamoja na malengo ya kimkakati ya pamoja ya muungano huo katika hatari ya kusambaratika.

Gazeti la The Economist limeandika kuwa: Njaa ya Marekani ya kuimeza Greenland inaweza kugharimu zaidi ya kisiwa na hatimaye kusambaratisha muungano wa bara zima ambao umejengwa kwa zaidi ya miaka 75.

Rais Donald Trump wa Marekani anasema Greenland ni muhimu kwa usalama wa taifa wa Marekani kutokana na kuwepo kwake katika eneo la kistratijia, na utajiri wake mkubwa wa madini, na anasisitiza kuwa, ikilazimu, atatumia nguvu kuinyakua. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *