Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelikosoa Kongamano la Uchumi la Dunia kwa kufuta mwaliko wake wa kuhudhuria Mkutano wa Davos.

Abbas Araqchi jana usiku alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X akisema: Uamuzi huo umechukuliwa na Kongamano la Uchumi la Dunia (WEF) kwa kutegemea uongo na mashinikizo ya kisiasa ya Israel na waitifaki wake wa Marekani.  

Kongamano la Uchumi la Dunia limesema kuwa mwaliko wake kwa Araqchi umeondolewa ukiashiria operesheni za Iran dhidi ya mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi, ambapo makundi ya kigaidi yaliwalenga askari usalama, raia na kuharibu mali za umma.

Araqchi alikuwa amepangiwa kuzungumza leo Jumanne katika kongamano hilo huko Uswisi. 

Abbas Araqchi  amesisitiza kuwa serikali ya Iran ilibidi kuwalinda watu dhidi ya “magaidi wenye silaha na mauaji ya mtindo wa kundi la Daesh (ISIS) yanayoungwa mkono waziwazi na Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad).” 

Araqchi amesema: Kongamano la Uchumi la Dunia (WEF) limemfutia mwaliko wake ingawa “mauaji ya kimbari ya Israel  dhidi ya Wapalestina na kuuliwa kwa umati watu wasio na hatia 71,000 hayakulifanya kongamano la Davos limefute mwaliko wowote uliotolewa kwa maafisa wa Israel.”

Kongamano la Uchumi la Dunia limebatilisha mwaliko aliopewa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi kuhudhuria mkutano wa Davos nchini Uswisi, kufuatia jibu la Tehran kwa machafuko na ghasia za karibuni zilizoungwa mkono na  Marekani na Israel nchini Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *