Yalcin ametoa wito wa kusitishwa mapigano mara moja, kushtakiwa wahusika na kesi za uhalifu wa kivita, na kufanikisha suluhisho la mataifa mawili.

Chama tawala cha Uturuki AK , kimekosoa kampeni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza kwa kuzitaja kama mauaji ya halaiki, huku Naibu Mwenyekiti wake wa Haki za Binadamu, Hasan Basri Yalcin, akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na kuahidi mshikamano wa Ankara na Wapalestina.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika Kituo cha Mpaka cha Rafah Jumatatu, Yalcin alisema Israel inaendesha ukandamizaji wa kabila kwa kuizingira Gaza, kusababisha maelfu ya watu kuhama, na kulenga raia wasio na hatia.

“Hii si vita dhidi ya ugaidi — haya ni mauaji ya watu wasio na hatia,” alisema. “Hadi sasa, raia 62,000 wamepoteza maisha kutokana na mashambulizi ya Israel, kati yao angalau watoto 20,000. Watu 10,000 zaidi wako hawajulikani waplipo na wengine wapo chini ya vifusi.”

Yalcin aliituhumu Israel kuharibu asilimia 80 ya majengo ya Gaza, ikiwemo hospitali, shule, na misikiti, na kuwafukuza watu asilimia 90 ya wakazi wa ukanda huo. Alidai serikali za Magharibi zimefumba macho kwa ukatili huo kutokana na ushawishi wa vikundi vya kupigania maslahi ya Israel.

“Mauaji haya ya halaiki hayawezi tena kufichwa,” alisema. “Taasisi za kimataifa hazitekelezi wajibu wao, huku miji mingi ya Magharibi ikibaki mateka wa kampeni za Israel.”

Wito kwa Ulimwengu wa Kiislamu

Akihutubia jamii kubwa ya Waislamu, Yalcin aliwataka kuungana na kuwaonya kwamba ukosefu wa mshikamano na mgawanyiko utanufaisha maslahi ya Israel pekee.

“Simameni na ndugu zenu walioteswa. Mkishindwa kufanya hivyo, wale wanaoshambulia Gaza leo watakulenga wewe kesho,” alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *