Watengenezaji wa magari wa Ujerumani wamekuwa wakijikongoja kwa zaidi ya muongo mmoja sasa. Mwanzoni mwa mwaka 2025 hata hivyo takwimu zilionesha kuwa kampuni kubwa ya magari ya Ujerumani Volkswagen, inauza magari mengi ya umeme. Sura ya Ujerumani inaangazia ikiwa sasa sekta hiyo muhimu inaelekea kupona au la.