Wafanyikazi katika uwanja wa ndege wa Ndjili jijini Kinshasa nchini DRC wameripotiwa kukamatwa kutokana na tukio kubwa la usiku wa Alhamisi ya Septemba tarehe 11 ambapo ndege ya Rais ilisubiri angani kwa karibia saa nzima kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na tukio hilo, ndege zengine zilicheleweshwa kuanza safari zao. Mkuu wa mamlaka ya usafiri wa angaa na manaibu wake walikamatwa na kuhojiwa na polisi.

Uwanja huo mkubwa wa ndege nchini DRC ulikumbwa na tukio la kukatika kwa umeme kwa zaidi ya saa nne wakati pia Jenereta kwenye uwanja huo zikikumbwa na hitilafu.

Ndege kadhaa za kimataifa zililazimika kutua katika nchi jirani ya Brazzaville, ndege zilizokuwa zikiondoka Kinshasa zikicheleweshwa kwa zaidi ya saa tatu.

Ndege ya Rais Félix Tshisekedi iliathirika kwenye tukio hilo wakati ikikaribia kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Ndjili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *