Mapigano yameanza tena mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). FARDC inapambana na wapiganaji wa AFC-M23 katika maeneo kadhaa. Mapigano haya yazuka wakati duru mpya ya mazungumzo imekamilika hivi punde huko Doha.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili, Septemba 21, waasi walichukua udhibiti wa Nzibira, mji wa kimkakati wa mkoa wa Kivu Kusini, kwenye makutano ya maeneo ya Mwenga na Shabunda, kulingana na vyanzo kadhaa vya ndani vilivyowasiliana na RFI.

Mapigano yalizuka mapema Jumapili, Septemba 21, mwendo wa saa 9:00 usiku, huko Nzibira, mji wa madini katika mko wa Kivu Kusini.

Wapiganaji walifanikiwa kuingia katikati mwa mji, lakini mapigano mapya hayako katika mkoa wa Kivu Kusini pekee.

Katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mapigano pia yalitokea Jumapili asubuhi karibu na Katobi, katika eneo la Walikale. Miliyo ya risasi na zana nzitio nzito na milipuko ilisikika takriban kilomita ishirini kutoka Pinga, jiji kubwa la mkoa huo.

Waasi wa AFC/M23 ambao awali walirudishwa nyuma siku ya Jumamosi,  walirudi kujaribu kuuteka tena mji huo. Kulingana na vyanzo vya ndani, tangu Ijumaa, jeshi la Kongo limekuwa likishambulia ngome zao karibu na Bibwe, katika eneo la Masisi, pia katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Mazungumzo ya kusitisha mapigano huko Doha na Washington yanakabiliwa na tishio. Katika taarifa, jeshi limetoa wito kwa wanajeshi wake, waliochukuliwa mateka au waliosajiliwa katika safu ya AFC/M23, kugeuza silaha zao dhidi ya vuguvugu hilo la waasi.

Haya yote yanakuja wakati wajumbe wa serikali na AFC/M23 waliondoka Doha mwishoni mwa juma lililopita.

Lakini timu ya upatanishi badi ina matumaini. Afisa wa Qatar, aliyewasiliana na RFI, amesema kuwa majadiliano yanaendelea mtandaoni na yataanza tena Doha baada ya wiki mbili, baada ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

“Miezi miwili baada ya makubaliano ya Doha na miezi mitatu baada ya makubaliano ya Washington, ni wazi kuwa hali imezorota”, anabainisha Rostin Manketa wa shirika la kutetea haki za binadamu la la Voix des sans voix.

Leo, kusema ukweli, watu wamekata tamaa. Uhasama unaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *