
Bila kusubiri matokeo rasmi kutangazwa, Rais anayemaliza muda wake Lazarus Chakwera, ambaye bado alikuwa akilaani udanganyifu katika uchaguzi jana, Jumanne, Septemba 23, amekiri kushindwa na kumpongeza mpinzani wake na mtangulizi wake, Peter Mutharika. Miaka mitano baada ya kutimuliwa mamlakani, Mutharika sasa anajiandaa kushika tena hatamu uongozi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Lazarus Chakwera amepongeza utendaji kazi wa Tume ya uchaguzi huku akitaka uchunguzi kamili na wa wazi kuhusu kasoro zilizobainika katika baadhi ya majimbo ufanyike. “Peter Mutharika tayari ana anaongoza kwa kishindo,” amekiri.
Kulingana na takwimu za awali, Peter Mutharika alipata zaidi ya 60% ya kura, ikilinganishwa na karibu theluthi moja ya Chakwera. Ushindi wa kishindo, unaofungua njia ya kurejea madarakani, miaka mitano baada ya kuondoka ikulu ya rais.
“Kukabidhiana madaraka kwa amani”
Lazarus Chakwera ambaye ni chungaji mwenye umri wa miaka 70, aliingia madarakani baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa mwaka 2019. Aliahidi kukabidhiana madaraka kwa amani, licha ya mamlaka ya muhula uliokuwa na matatizo makubwa ya kiuchumi: zaidi ya 70% ya wakazi wanaishi chini ya dola 2 kwa siku, kulingana na Benki ya Dunia, jambo ambalo bila shaka lilikuwa na uzito kwa wapiga kura.