#HABARI: Idadi ya waliofariki kutokana na kuporomoka kwa jengo la shule nchini Indonesia imefikia 54, mamlaka imesema, huku waokoaji wakiendelea kutafuta zaidi ya watu kumi na wawili waliopotea.

Mamia ya wanafunzi, wengi wao wakiwa wavulana, walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya maombi katika shule ya bweni ya Kiislamu ya Al Khoziny huko Java Mashariki ilipoporomoka Jumatatu iliyopita ilipokuwa ikijengwa.

Shirika la kukabiliana na majanga nchini Indonesia linasema kuwa hilo ndilo janga baya zaidi nchini humo mwaka huu.

Waokoaji wanatarajiwa kukamilisha zoezi lao la kuwatafuta waathiriwa 13 walionasa chini ya vifusi kufikia mwisho wa siku.

Wachunguzi bado wanatafuta sababu ya kuanguka kwa jengo.

Baadhi ya viongozi walisema jengo hilo la ghorofa mbili lilianguka kwa sababu msingi wake haukuwa thabiti.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *