Kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja, jina la Joseph Kabila lilitulia kimya ndani na nje ya DRC. Rais huyo wa zamani alijipeleka uhamishoni mwenyewe bila kujulikana kwa uhakika alikuwa wapi au alikuwa anafanya nini.
Lakini kufikia mwezi Aprili 2025, mara alianza kusikika akichangia siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kufikia mwezi Mei, akatikisa siasa za nchi hiyo kwa kurejea nchini, japo Mashariki mwa nchi ambako anadaiwa kuwa na uungwaji mkono au ushawishi na makundi ya waasi yanayopigana na serikali.
Katika kesi inayoonekana kuharakishwa, Mahakama ya kijeshi ilimtia hatiani Kabila bila kuwepo kwa uhalifu mkubwa – ikiwa ni pamoja na uhaini na uhalifu wa kivita na kumpa hukumu ya kifo – kuhusiana na madai ya kushirikiana na waasi wa M23 ambao walienea katika maeneo ya Kivu Kaskazini na Kusini mapema mwaka huu.
Mahakama pia ilimuamuru Kabila kulipa fidia ya dola bilioni 29 kwa DRC, pamoja na dola bilioni 2 kwa jimbo la Kivu Kaskazini nchini humo na dola bilioni 2 kwa Kivu Kusini. Kabila amekana mashtaka hayo.
Hukumu hii inamaanisha nini ?
Waangalizi wengi wa kimataifa na DRC wanasema kesi hiyo ilikuwa na muelekeo wa wazi wa kisiasa na kuibua maswali kuhusu utaratibu unaostahili na utekelezwaji wa vyombo vya mahakama. Human Rights Watch ilisema kuwa kesi hiyo inaonekana kama kisasi kinachotishia athari kubwa kwa sheria ya nchi.
‘‘Hukumu iliyotolewa kwa rais Kabila kutokana na madai ya kuwa na uhusiano na M23 sio tu ni maonesho ya haki lakini pia ni ukiukaji mkubwa wa tamko la kanuni,’’ alisema Lumumba Kambere, msemaji wa M23, Kivu ya Kaskazini.
Lakini Kabila sio tu rais wa zamani kwenye karatasi. Ana mitandao ya muda mrefu ndani ya wasomi wa kisiasa, kijeshi na kiuchumi nchini humo, na mwaka wa 2025 alijitokeza hadharani ndani na karibu na Goma inayoshikiliwa na waasi – kuashiria ufikiaji na ushawishi katika maeneo ya mashariki ambapo M23 na wahusika wengine wanafanya kazi.
Kwa hiyo kumhukumu kifo si adhabu tu; inaunda upya motisha za wahusika wenye nguvu mashinani.
Nani atamkamata?
Hukumu kwa kutokuwepo kwake inaweka amri ya kudumu, inayotekelezeka kwa kukamatwa kwake na madeni makubwa ya kifedha.
Kiuhalisia, hata hivyo, hatari ya moja kwa moja ya Kabila inategemea kama yuko katika eneo linalodhibitiwa na wahusika walio tayari kumkabidhi kwa DRC, na kama mataifa jirani au washirika wanamlinda inamaanisha sio jambo rahisi kutiwa pingu huko aliko.