Mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina na usitishwaji vita huko Gaza yamepangwa kuanza leo Jumatatu, Oktoba 6, katika eneo la mapumziko la Bahari Nyekundu la Sharm el-Sheikh nchini Misri. Maafisa wa Israel, viongozi wa Hamas, na wapatanishi wa Misri, Qatar na Marekani watahudhuria.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ujumbe wa Hamas ndio wa kwanza kuwasili Misri, anaripoti mwandishi wetu mjini Cairo, Alexandre Buccianti. Unaongozwa na Khalil Al-Hayya, ambaye aliwasili Misri jana usiku. Mikutano hii, iliyopangwa kufanyika leoJumatatu huko Sharm el-Sheikh, mashariki mwa Sinai, ni ya kwanza kuhudhuriwa na mpatanishi mkuu wa Hamas tangu Israel ilipomlenga yeye na viongozi wengine wa vuguvugu hili la Kiislamu katika shambulio huko Doha mwezi uliopita. Wakati uo kndi la wanamgambo la Hamas  liliripoti vifo sita.

Khalil Al-Hayya alizungumza jana, Jumapili, kwenye kituo cha televisheni ya Qatar Al-Araby, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonekana tangu mashambulizi ya Israel. Katika hotuba hii ya televisheni iliyorekodiwa awali, hakutaja mpango wa Marekani kwa Gaza au mazungumzo yanayoendelea, amebainisha Alice Froussard wakitengo cha kimataifa cha RFI. Alitaja kifo cha mtoto wake wa kiume, aliyeuawa pamoja na wengine watano katika shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa na Israel ambalo liliwalenga maafisa wa Hamas huko Doha mapema mwezi Septemba. “Kumpoteza mwanangu, wenzangu, mkurugenzi wa ofisi yangu, na vijana wanaonizunguka (ni) maumivu makubwa,” alisema. Katika video hii, iliyorushwa wakati mazungumzo yakifunguliwa, na kwa sauti ya uchochezi kwa Israeli, Khalil Al-Hayya kimsingi analenga kuwatuliza Wapalestina huko Gaza, kana kwamba mpatanishi mkuu wa Hamas anawasilisha hali ya utulivu, mrengo wa kisiasa wa kundi hilo unaowajali watu wake katika eneo la pwani.

Ujumbe wa Israel unatarajiwa kuwasili baadaye leo huko Sharm el-Sheikh, mji wa ishara ambapo mazungumzo na makongamano mengi ya amani ya Mashariki ya Kati tayari yamefanyika. Siku ya Jumapili jini Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alikutana na ujumbe unaoelekea Misri kujiandaa kwa majadiliano hayo, anaripoti mwandishi wetu mjini Jerusalem, Frédérique Misslin. Ron Dermer, Waziri wa Masuala ya Kimkakati anayesimamia hali ya mateka, anaongoza timu ya mazungumzo ya Israel. Ameandamana na wakuu wawili wa idara za kijasusi, Shin Bet na Mossad. Katika ngazi ya kisiasa, Benjamin Netanyahu ameweza kuweka kundi lake la mrengo wa kulia kusubiri hadi mateka waachiliwe. Mkutano huo umelenga katika awamu za mpango wa Marekani wenye vipengele ishirini (Hamas kupokonywa silaha na kuondoa Gaza). Kwa mawaziri wenye msimamo mkali katika muungano unaotawala, baadhi ya hoja hazijadiliwi na zinatishia kuiangusha serikali.

Kwa mazungumzo halisi, Israel na Hamas watazungmzo sio moja kwa moja, lakini watakuwa katika vyumba tofauti. Wapatanishi wa Misri na Qatar watakuwa wakikutana na kila upande kwa nyakati tofauti. Wamarekani hao, akiwemo mjumbe wa Rais wa Marekani Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, wanatarajiwa kuungana nao siku ya Jumanne.

Hamas lazima kwanza iwarudishe mateka zaidi ya ishirini wanaoaminika kuwa hai na mabaki ya wale waliofariki wakiwa kizuizini. Kulingana na vyanzo vya Hamas, mabaki ya mateka waliofariki yanakusanywa kwa sasa. Operesheni hii itachukua muda, na tarehe ya mwisho kukubaliwa na Washington. Hamas, hata hivyo, imeonyesha kuwa mateka walio hai wanaweza kuachiliwa kwa haraka. Kwa hivyo masharti ya shughuli hizi zote lazima yafafanuliwe.

Kwa kubadilishana na mateka, wafungwa 250 wa Kipalestina waliohukumiwa kifungo cha maisha wataachiliwa, pamoja na Wagaza 1,700 waliozuiliwa baada ya Oktoba 7, 2023. Bila shaka kutakuwa na mijadala mikali kuhusu majina kwenye orodha hii.

Hatimaye, mstari wa kuondoka kwa wanajeshi wa Israel utajadiliwa. kuondoka kwa wanajeshi wa Israel kulitangazwa kama hatua kwa hatua. Kwa mujibu wa vyanzo ndani ya vuguvugu la Kiislamu, Hamas imepokea hakikisho la Marekani kupitia Qatar kuhusu kuondoka kwa wanajeshi wa Israel katika mji wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *