
Ni baada ya waziri wa zamani wa utalii na masuala ya kale wa Misri, Khaled el-Anani, kuteuliwa na bodi ya utendaji ya shirika hilo. Iwapo atathibitishwa na mkutano mkuu wa UNESCOmwezi ujao, el-Anani atarithi shirika ambalo linakumbwa na msukosuko kufuatia uamuzi wa hivi karibuni wa utawala wa Trump wa kuiondoa Marekani, jambo linaloashiria upungufu wa bajeti katika shirika hilo linalojulikana zaidi kwa maeneo yake ya Urithi wa Dunia kote duniani. El-Anani alionekana kuwa mgombea anayepewa nafasi kubwa ya kushinda nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na alishinda katika zoezi la uoigaji kura siku ya Jumatatu dhidi ya mpinzani wake pekee, Firmin Edouard Matoko, mchumi kutoka Jamhuri ya Kongo ambaye alihamasisha elimu katika kambi za wakimbizi.Uamuzi wa bodi, inayowakilisha nchi wanachama 58 kati ya 194 wa shirika hilo, unatarajiwa kukamilishwa katika mkutano wa Mkutano Mkuu wa UNESCO utakaofanyika Uzbekistan mwezi ujao.