Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limelazimika kupunguza karibu ajira 5,000 tangu mwanzoni mwa mwaka huu, huku kukiwa na upungufu mkubwa wa ufadhili wa misaada ya kimataifa, Kamishna wake Mkuu amesema leo Jumatatu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Bila ufadhili wa ziada, UNHCR itakabiliwa na “mwanzo mgumu sana wa mwaka 2026,” Kamishna Mkuu amezambia nchi wanachama. Shirika hilo la Umoja wa Mataifa, linalokabiliwa na kupunguzwa kwa fedha kutoka Marekani na mataifa mengine kadhaa, linaweza kukosa pesa taslimu.

“Takriban wafanyakazi wenzetu 5,000 wa UNHCR tayari wamepoteza kazi mwaka huu,” Filippo Grandi amesema wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa kamati kuu ya shirika hilo, akisisitiza kwamba “hii inawakilisha zaidi ya robo ya wafanyakazi.”

Shirika hilo lilitangaza kupunguzwa kwa nafasi kati ya 3,500 na 4,000 mwaka huu. Idadi hii sasa imefikia karibu 5,000, Bw. Grandi amesema mwanzoni mwa mkutano wa Kamati Tendaji ya UNHCR. Na anatarajia kwamba kupunguzwa zaidi kunatarajiwa.

Mabadiliko au kufungwa kwa ofisi za UNHCR kumeshuhudiwa katika ofisi 185 za UNHCR duniani kote. Huku shirika hilo likiomba zaidi ya dola bilioni 10, kiasi ambacho kiliidhinishwa na nchi wanachama mwaka jana, shirika hilo la Umoja wa Mataifa linatarajia kupokea dola bilioni 3.9 pekee ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Hii inawakilisha kushuka kwa dola bilioni 1.3 kwa mwaka mmoja na hali ambayo haijaonekana katika muongo mmoja, kiwango ambacho UNHCR ingeweza kutarajia.

“Sidhani kama huu ni mzozo wa kifedha,” Bwana Grandi ameongeza. Ameshutumu “chaguo za kisiasa ambazo zina athari mbaya za kifedha.” Itachukua miaka kurejesha utaalam ndani ya shirika hili, lakini anaahidi kwamba UNHCR itaendelea kwa uthabiti msaada wake kwa wakimbizi. Kwa mwaka 2026, UNHCR inahitaji dola bilioni 8.5.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *