
Othman ameongeza kusema kuwa, kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ilitokana na hekma na juhudi kubwa za watangulizi katika kustawisha amani ya kweli Zanzibar na kwamba ni vyema nchi ifanye uchaguzi wa haki na usawa.
Aidha amesema kwamba iwapo atashinda urais, serikali yake haitoruhusu biashara ama uwekezaji kwa wageni unaoweza kufanywa na wenyeji na badala yake itawezesha wananchi kiutalamu, nyenzo na rasilimali ili waweze kufanya shughuli hizo na kuwapatia ajira na kipato chenye manufaa.