#HABARI: Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Sita imefanya mageuzi makubwa ya maendeleo katika Wilaya ya Nyamagana, na kwamba katika awamu ijayo itahakikisha maendeleo hayo yanazidi kuimarika katika sekta zote zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni Nyamagana jijini Mwanza, Dkt. Samia amesema Serikali imeweka mkazo mkubwa katika sekta ya afya, kwa kujenga na kukarabati vituo vya afya na zahanati katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, pamoja na kuimarisha huduma za hospitali kuu ya wilaya.

“Tumeongeza upatikanaji wa huduma bora za afya, tunajenga vituo vipya, tunaajiri watumishi wa afya, na sasa mwananchi wa Nyamagana hapaswi kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma,”amesema Dkt. Samia

Katika sekta ya elimu, Dkt. Samia ameeleza kuwa Serikali imeongeza fedha za kugharamia mpango wa elimu bila ada, sambamba na ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari ambazo zimepunguza msongamano wa wanafunzi.

Akizungumzia maji safi na salama, Dkt. Samia amesema miradi mikubwa ya maji imefanyika kwa mafanikio, na upatikanaji wa huduma hiyo umeimarika kwa kiwango kikubwa, jambo lililopunguza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa vijijini na mijini.

Kuhusu miundombinu, alisema Serikali imeendelea kuboresha barabara ndani ya Jiji la Mwanza, hususani Nyamagana, ili kurahisisha usafiri na biashara.
“Tumejenga barabara za lami, tumeimarisha barabara za mitaa, na sasa tunapanua miundombinu ya mitaa kwa ajili ya kukuza uchumi wa wananchi wetu,” alisema Dkt. Samia.

Katika sekta ya uchumi na uwezeshaji wananchi, amebainisha kuwa Serikali imeongeza mikopo ya asilimia 10 kupitia halmashauri kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, hatua inayowasaidia kujiajiri na kukuza uchumi wa kaya.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *