Mkusanyiko huo unafanyika wakati Israel ikikumbuka miaka miwili tangu shambulio hilo lililotumbukiza eneo la Mashariki ya Kati katika vita vikali.

Kumbukumbu hiyo inafanyika huku wajumbe wa Israel na wa kundi la Hamas wakiendelea na mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja ya kusitisha mapigano yanayofanyika nchini Misri.

“Tarehe 7 Oktoba, saa 12 asubuhi, kila kitu kilibadilika. Kote nchini Israel, yakiwemo makaazi yetu hapa. Ilikuwa siku mbaya zaidi katika maisha yetu, watu 62 kutoka hapa waliuawa siku hiyo hiyo. Wengine wawili waliuawa baadaye na watu 19 walitekwa nyara.”

Kumbukumbu hiyo imeandaliwa na familia zilizopoteza wapendwa wao, tofauti na hafla rasmi itakayofanywa wiki ijayo na serikali kwa mujibu wa kalenda ya Kiebrania.

Mgawanyiko huu unaonyesha tofauti kubwa kuhusu uongozi wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye anakosolewa na wengi kwa kushindwa kuhakikisha usitishaji mapigano, hatua ambayo ingefungua fursa ya kuachiliwa kwa mateka waliobaki mikononi mwa Hamas.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *