Wakati huu makabiliano yakiendelea kuripotiwa nchini DRC, suala ibuka ni iwapo awamu ya sita ya majadiliano kati ya kundi waasi AFC/M23 na serikali ya Kinshasa yatarejelewa juma hili jijini Doha kama ilivyotangazwa na mpatanishi nchi ya Qatar.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hadi kufikia sasa badi haijafahamika ikiwa majadiliano hayo yatafanyika, taarifa ya idhaa ya RFI, huenda majadiliano hayo yakarejelewa hata hivyo bado kuna mgawanyiko mkubwa, ambapo pande zote zinatofautiana haswa kuhusu utaratibu wa kusitisha mapigano.

Majadiliano ya juma hili yanalenga kuboresha maandishi yatakayoanzisha utaratibu wa kudumu wa usitishaji mapigano.

Zaidi ya hayo, wajumbe walitakiwa kuwa wamekutaka Oktoba 3, ikizingatiwa hatua zilizopigwa kwenye maandishi hayo, kwa mujibu wa vyanzo vya RFI, hata hivyo sula ibuka ni jukumu la MONUSCO katika utaratibu wa ufuatiliaji wa usitishaji mapigano.

Kundi la AFC/M23 linasema halina imani na ujumbe huo wa MONUSCO, ambao kundi hilo linaitazama kama kikosi kilichofeli

Kwa upande mwingine, Kinshasa, inasisitiza kuwa ni sharti MONUSCO ifanye kazi kulingana na wajibu iliopewa na baraza la usalama la UN, wajibu unaojumuisha vita dhidiya M23.

Iwapo pande zote zitaafikiana kuhusu toleo la mwisho la maandishi, basi hatua hiyo itafungua njia ya kuanza kwa awamu ya sita ya majadiliano baadaye wiki hii

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *