#UPDATE: Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Antipas Lissu, inaendelea katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo kwa sasa, imeahirishwa kwa muda na inatarajia kuendelea tena Alasili hii.
Kilichojiri, Lissu ameendelea kumuuliza maswali dodosi (cross examination) shahidi wa Jamhuri ACP George Wilbert ambaye alianza kutoa ushahidi wake hapo jana.
Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, shtaka linalotokana na maneno aliyodaiwa kuyatoa kuhusu kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.