Kulingana na azimio hilo, nchini ya kifungu 119, nchi wanachama zimejitolea kushirikiana katika kukuza michezo na shughuli za kitamaduni, kama nyenzo ya kukuza utambulisho wa jumuiya hiyo.

Mwezi Agost 2025, Tanzania, Kenya na Uganda, ziliandaa kwa pamoja michuano ya CHAN 2024, ambayo ni maalumu kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani.

Wiki kadhaa baadaye, Rwanda iliandaa michuano ya kimataifa ya mbio za baiskeli, zilizofanyika  kutoka Septemba 21 hadi 28, 2025.

“Nchi zetu zimeonesha, sio tu uwezo wake wa kuandaa michuano yenye hadhi ya kimataifa, bali utajiri wa kitamaduni, uzuri asilia na ukarimu wa watu wa Afrika Mashariki,” alisema Iman.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *