Nchini Burkina Faso, serikali imetangaza kukamatwa kwa watu wanane, wakiwemo wageni wanne, ikiwa ni pamoja na mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la International NGO Safety Organisation (INSO). 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirika hili, ambalo lina utaalam wa kukusanya habari kutoka mashinani ili kusaidia mashirika ya kutoa misaada kibinadamu, limesimamishwa tangu mwisho wamwezi Julai. Wafanyakazi hao wanane wanatuhumiwa kwa “ujasusi na uhaini.” Shirika hili, ambalo limesema kuwa “linafutilia mbali  kabisa shutuma hizi,” limesema kuwa linafanya kila juhudi kuhakikisha wafanyikazi wake wanaachiliwa.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliohudhuriwa na msemaji wa serikali ya Burkina Faso Gilbert Ouédraogo, Waziri wa Usalama, Mahamadou Sana, ameelezea uchunguzi uliofanywa tangu kukamatwa kwa mkurugenzi wa INSO nchini Burkina Faso, Mfaransa Jean-Christophe Pégon, mwishoni mwa mwezi Julai. INSO inashutumiwa haswa kwa kukusanya taarifa kwa mataifa ya kigeni kuhusu mienendo ya jeshi na makundi ya kigaidi, anaeleza Mahamadou Sana. “INSO ilitumia muda wake kukusanya taarifa kuhusu maeneo ya operesheni pamoja na uingiliaji kati wa vikosi vya ulinzi na usalama mashinani.”

Mamlaka za kijeshi pia zinashuku INSO kwa kuendelea kufanya kazi licha ya kusimamishwa kwa shughuli zake kwa agizo mnamo Julai 31, 2025, anabainisha Mahamadou Sana. “Licha ya kusimamishwa kazi, baadhi ya maafisa wa INSO waliendelea kufanya shughuli kwa siri kama vile kukusanya taarifa na mikutano ya ana kwa ana au mtandaoni.”

Mbali na mkurugenzi wa shirika hilo nchi Burkina Faso, wafanyakazi saba wa mashirika yasiyo ya kiserikali, naibu mkurugenzi, ambaye ni raia wa Ufaransa mwenye asili ya-Senegal, mkurugenzi wa programu, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Czech, raia wa Mali, na raia wanne wa Burkina Faso walikamatwa. Mamlaka zinaonyesha kwamba watafikishwa mbele ya mwendesha mashtaka wa Burkina Faso kwa “ujasusi na uhaini.”

Katika taarifa yake, INSO imesema: “Kuunganisha kazi yetu ya kuimarisha usalama wa kibinadamu na shughuli za kijasusi sio tu makosa, lakini kutaongeza tu hatari kwa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *