#HABARI: Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, amesema anapanga kufanya “mazungumzo ya kitaifa” na makundi mbalimbali leo hii, baada ya waandamanaji vijana kumpa saa 48 akubali madai yao au wataitisha maandamano ya kitaifa.
Amesema kuwa mazungumzo yaliyopangwa kufanyika mchana yatashirikisha viongozi wa kiroho, wanafunzi, wawakilishi wa vijana, na makundi mengine. Jumatatu, Rajoelina alimteua Jenerali wa Jeshi Ruphin Fortunat Zafisambo kuwa Waziri Mkuu mpya, wiki moja baada ya kuwafuta kazi mawaziri wake wote katika hatua ya kushughulikia malalamiko yaliyochochea maandamano ya Septemba 25.
Hata hivyo, mabadiliko hayo hayajawatuliza waandamanaji, ambao awali walijitokeza mitaani kulalamikia uhaba wa maji na umeme katika taifa hilo maskini la Afrika, lakini sasa wanataka Rais Rajoelina ajiuzulu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania