Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Japani umefanya ziara katika maeneo yanayosimamiwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA) kwa lengo la kutathmini fursa na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Japani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, James Maziku amesema ziara hiyo imelenga kuonesha maeneo ya uwekezaji na sera rafiki za Tanzania, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuvutia wawekezaji wa kimataifa.
#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi