Wanaharakati sita wa Afrika Kusini ambao waliwekwa kizuizini huko Israel baada ya kutekwa nyara kutoka katika msafara wa kimataifa wa meli kwa jina la Global Sumud Flotilla kuelekea Gaza wamesimulia hadithi za kusikitisha kuhusu walichopitia wakiwa mikononi mwa wanajeshi wa Israel.

Mandla Mandela, mjukuu wa hayati Rais wa Afrika Kusini na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi, mzee Nelson Mandela jana aliuambia mkutano na wanahabari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo karibu na Johannesburg muda mfupi baada ya kutua nchini humo kwamba:” Wanajeshi wa Israel waliwafunga pingu za nyaya huku mikono yao ikiwa nyuma ya migongo.”

Amesema Itamar Ben-Gvir Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel alifika na kuwatolea maneno makali akisema: ” Nyie mnaunga mkono wauaji wa watoto na kisha kutuita magaidi.” Mandela amesema hata wanaharakati hao hakuwamnyamazia kimya Itamar na alikabiliwa na nara za wanaharakati hao wa Afrika Kusini waliokuwa wakisema “Free Free Palestine. Waliendelea kumkaripia kwa ukali Itamar ambapo walimwambia sisi si wauaji wa watoto; nyinyi ndio ndio mnaouwa watoto, na Ben-Gvir hakuwa na majibu.

Naye Dakta Fatima Hendricks mwanaharakati wa msafara wa kimataifa wa Gaza Flotila miongoni mwa waliotiwa mbaroni na Israel amesema kuwa: Wanajeshi wa Israel waliingia katika chumba walichokuwa wakishikiliwa na kuwashambulia wanawake wawili nje ya mlango wa seli hiyo ambapo walikuwa wakijaribu kupata godoro. 

Dakta Fatima Hendricks anaendelea kusimulia, kulikuwa na takriban wanawake 10 au 12 kwenye seli yao, lakini wanajeshi wa Israel waliwajibu kwa aina hii ya ukatili ulipoindukia walipowasili mahali hapo: “Hawa ni wanajeshi wa kazi wa Kizayuni ambao hawajui chochote isipokuwa mabavu.

Amesema wanajeshi wa Israel walielekeza bunduki zao katika vipaji vya nyuso zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *