Kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu inaendelea leo ambapo shahidi wa pili wa upande wa Jamhuri, Inspekta John Kaaya ataulizwa maswali ya dodoso na mshitakiwa.
Kesi hiyo inasikilizwa katika Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, chini ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi