Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kukamilisha mchakato wa Katiba mpya ili kulinda tunu za taifa zikiwemo amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza Butiama, mkoani Mara, Dkt. Samia amesema mchakato huo ni matakwa ya Watanzania na utaendelezwa katika awamu ya sita baada ya kusimama awali.
Amesema Serikali itaendelea kujenga taifa jumuishi na lenye ustawi kwa kuimarisha sekta za kijamii na kiuchumi, sambamba na kudumisha misingi iliyoachwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates